WATUMISHI WAPYA MPRU WAPATIWA MAFUNZO ELEKEZI (INDUCTION COURSE)
Jumanne, Januari 14, 2025 Dar es Salaam
Watumishi wapya kutoka Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU) wamepatiwa mafunzo elekezi (induction course) kuwawezesha watumishi wapya kuelewa sheria, kanuni, taratibu na maadili katika utumishi wa umma ambapo mafunzo hayo yalifanyika katika ukumbi wa Chuo cha Utumishi wa Umma uliopo Dar es Salaam.
Mafunzo hayo yaliyoendeshwa na Makamu Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Dkt. Charles Rwekaza yametolewa kwa siku tano kuanzia Januari 13-17, 2025. MPRU iliwakilishwa na watumishi kutoka Makao Makuu na Kituo cha Dar es Salaam (DMRS), Kituo cha Mtwara (MBREMP) na Kituo cha Mafia (MIMP).
Mafunzo hayo yaliyowezeshwa na Idara ya Utawala ya MPRU yanalenga kuwawezesha watumishi kufanya kazi kwa uadilifu katika Utumishi wa Umma na Serikali kwa ujumla. Watumishi wapya kutoka Makao Makuu walikuwa ni Halima Tosiri (Afisa Masoko), Ivan Kimaro (Afisa Uhusiano), John Mweluwe (Afisa Ugavi), Zuberi Issa (Dereva), Lustico P. Lyogo (Afisa Hesabu).
Kwa upande wa Kituo cha Dar es Salaam (DMRS) ni Gister Nkini (Mhifadhi Bahari), Kijoli Seleman (Mhifadhi Bahari), Yusuph Katwange (Dereva wa Boti) na kwa Kituo cha Mafia (MIMP) walikuwa ni Kulwa Mtaki (Mhifadhi Bahari), Ailars Peter (Mhifadhi Bahari).
Halikadhalika, kwa upande wa Mtwara (MBREMP) alikuwa ni Mustapha Issa (Mhifadhi Bahari).