WATUMISHI TACMP WAPATIWA MAFUNZO YA MFUMO MPYA WA MAKUSANYO YA NDANI ‘MRPS’
Ijumaa, Januari 24, 2025 Tanga
Timu ya Wataalam kutoka Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU) imefanya zoezi la mafunzo ya mfumo mpya wa ukusanyaji wa mapato wa ndani ujulikanao kama 'Marine Reservation and Payment System' (MRPS) kwa watumishi wa kituo cha Hifadhi ya Bahari ya Tanga Silikanti (TACMP) kilichopo Mkoani Tanga.
Mafunzo hayo yaliongozwa na Afisa Tehama Bw. Yusuph Rajabu kuwajengea uwezo watumishi wa TACMP kuhusianana na mfumo na utendaji kazi wake ambapo mfumo huo mpya wa MRPS unatarajia kuchangiza weledi na umakini katika vituo vya makusanyo na kuchochea kuongezeka kwa mapato ya ndani.
Aidha, mafunzo hayo yalipatwa kuhudhuriwa na wadau wajulikanao kama ’Friend of Maziwe’ ambao hujitolea kushiriki katika shughuli mbalimbali za uhifadhi katika Kisiwa cha Maziwe.