MIMP WAPATIWA MAFUNZO YA MFUMO MPYA WA MAKUSANYO YA NDANI ‘MRPS’
Jumamosi, Disemba 22, 2024 Mafia
Timu ya Wataalam kutoka Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU) imefanya zoezi la mafunzo ya mfumo mpya wa ukusanyaji wa mapato wa ndani ujulikanao kama MRPS kwa watumishi wa kituo cha Hifadhi ya Bahari ya Kisiwa cha Mafia (MIMP).
Mafunzo hayo yaliyoongozwa na Afisa Tehama Bw. Yusuph Rajabu aliyeongozana na msaidizi wake Bw. Abas Maige pamoja na Afisa Mapato Bi. Judith Kerengi walishirikiana kuhakikisha zoezi hilo linafanyika kikamilifu na watumishi wa MIMP kuweza kuuelewa mfumo huo ambao utachangiza weledi na umakini katika ukusanyaji wa mapato ndani ya Hifadhi ya Bahari ya Kisiwa cha Mafia.
Aidha, utumiaji wa mfumo huu wa Marine Reservation and Payment System (MRPS) ni hatua mojawapo ya kutimiza agizo la Serikali kupitia Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa ambapo alizitaka taasisi za umma ziweke mipango madhubuti ya kutumia mifumo ya kidijitali ambayo italeta mageuzi ya kiutendaji na kuifanya Tanzania kuendana na mapinduzi ya nne ya viwanda yanayotumia TEHAMA.