WATANZANIA WATAKIWA KULINDA RASILIMALI YA MIKOKO
WATANZANIA WATAKIWA KULINDA RASILIMALI YA MIKOKO

Ijumaa, Machi 07, 2025, Dar es Salaam

Mhifadhi Mkuu kutoka Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU) Bw. Godfrey Ngupula amewataka watanzania kwa nafasi yao kulinda mikoko kwani ni moja ya rasilimali muhimu katika Bahari.

Aliyasema hayo wakati akihojiwa na kituo cha redio cha Radio One na mtangazaji Abdullah Kilwa katika kipindi cha Kumepambazuka na Radio One ambapo mahojiano hayo yalifanyika katika Ofisi Kuu za MPRU zilizopo Upanga jijini Dar es Salaam.

“Nimuombe mtanzania popote pale ulipo kama upo karibu na mikoko linda mikoko kwani ni jambo zuri jiskie vibaya kukata mikoko jiskie kama unatenda dhambi kwasababu mkoko mmoja unafaida kubwa sana” alisema Ngupula.

Halikadhalika, Ngupula aliwataka pia watanzania kuwa wabunifu katika namna ya kutumia hizi rasilimali ili ziweze kutuletea faida na kuiongezea serikali mapato.