WANAFUNZI WA VYUO VIKUU MKOA WA DAR ES SALAAM WAPATIWA ELIMU KUHUSIANA NA FURSA ZILIZOPO KATIKA MAENEO YA UHIFADHI WA BAHARI
WANAFUNZI WA VYUO VIKUU MKOA WA DAR ES SALAAM WAPATIWA ELIMU KUHUSIANA NA FURSA ZILIZOPO KATIKA MAENEO YA UHIFADHI WA BAHARI

Jumamosi, 20 Julai 2024, Dar es Salaam.

Wanafunzi kutoka vyuo tofauti Mkoa wa Dar es Salaam wamepatiwa elimu kuhusiana na  shughuli mbalimbali zinazofanywa na taasisi ya Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu Tanzania (MPRU) ili kubaini fursa zilizopo kupitia shughuli zinazofanywa na taasisi hiyo kwa lengo la kujengewa uwezo wa kujiajiri watakapohitimu mafunzo yao.

Wanafunzi hao waliojiandikisha katika shirika lisilo la kiserikali la “Mutual Generation International (MGI)“  ambalo hutoa elimu ya kujitegemea kwa vijana ili kuweza kutambua fursa za ajira zinazowazunguka ili kujikwamua kiuchumi.

Mutual Generation International (MGI) ni Shirika lisilo la kiserikali linalohusika na kutoa elimu ya kujitegemea kwa vijana ili kuweza kutambua fursa za ajira zinazowazunguka ili kujikwamua kiuchumi.

Jumla ya İdadi ya wanafunzi kumi na tatu (13) walishiriki katika mafunzo hayo.