UFUNGUZI WA WARSHA YA MRADI WA UTATUZI WA CHANGAMOTO ZA UHIFADHI (PAMO-NBS) MAFIA
UFUNGUZI WA WARSHA YA MRADI WA UTATUZI WA CHANGAMOTO ZA UHIFADHI (PAMO-NBS) MAFIA

Jumanne, 25 Septemba 2024, Mafia

Kaimu Meneja wa Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu, Bw. Davis Mpotwa amefungua rasmi warsha yenye lengo la kutafuta ufumbuzi wa changamoto za Uhifadhi kwa kutumia maarifa ya asili kupitia mradi wa Participatory Modelling for Nature-Based Solutions (PAMO-NBS).

Warsha hiyo ya uzinduzi wa mradi huo ilifanyika Septemba 25, 2024 katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Hifadhi za Bahari ya Kisiwa cha Mafia (MIMP) iliyopo Wilayani Mafia, Mkoa wa Pwani.

Mradi huu unalenga kuimarisha juhudi za Uhifadhi kwa kuhusisha jamii na kutumia mifumo ya asili ya maarifa kama mbinu bora za kukabiliana na changamoto za mazingira.

Warsha hii imeandaliwa kwa ushirikiano kati ya Taasisi ya Sayansi za Bahari (IMS) na Kituo cha Ujerumani cha Utafiti wa Maswala ya Bahari ya Kitropiki (ZMT) na inatekelezwa kwa pamoja nchini Tanzania na Madagascar ikilenga kuleta suluhisho endelevu kwa masuala ya Uhifadhi wa mazingira na rasilimali za bahari.