TIMU YA WAFANYAKAZI WA MBREMP YAFANYA UOKOZI WA NYANGUMI (HUMPBACK WALE) KATIKA KIJIJI CHA MSANGA MKUU
TIMU YA WAFANYAKAZI WA MBREMP YAFANYA UOKOZI WA NYANGUMI (HUMPBACK WALE)  KATIKA KIJIJI CHA MSANGA MKUU

Jumanne, 20 Agosti 2024, Mtwara

Timu ya wafanyakazi wa Hifadhi ya Bahari ya Ghuba ya Mnazi na Maingiliano ya Mto Ruvuma (MBREMP) ikiongozwa na Mhifadhi Mfawidhi Dkt. Reidfred Ngowo imefanya zoezi la uokoaji lililofanikiwa kikamilifu wa Nyangumi  mwenye nundu (Humpback wale) aliyenaswa kwenye nyavu za uvuvi na kuvutwa ufukweni na wavuvii katika kijiji cha Msanga Mkuu kilichopo mkoani Mtwara.

Zoezi hilo la uokoaji lililofanyika Agosti 17, 2024 lilishirikisha wafanyakazi, mashirika ya ulinzi pamoja na wanajamii walifanikiwa kuondoa nyavu hizo kwa usalama, kutathmini majeraha yaliyoweza kumuathiri Nyangumi huyo pamoja na kumrudisha kwenye kina kirefu cha maji.

Aidha, licha ya changamoto kama vile ukubwa wa Nyangumi, hali ya hewa pamoja nahali ya kuchanganyikiwa kwa samaki huyo waokoaji waliweza kukamilisha zoezi la operesheni ya uokoaji kwa ukamlifu.

Halikadhalika, timu iliyoshiriki zoezi la uokoaji iliweza kujibu taarifa za kijasusi kuhusu Nyangumi huyo ambapo waliandaa ripoti na kupendekeza mbinu madhubuti ya kukabiliana na matukio mengine kama haya ikiwemo utoaji wa mafunzo zaidi kwa wafanyakazi, kupatiwa vifaa maalum vitakavyoweza kusaidia katika zoezi la uokaji pamoja na kuongeza ufahamu kwa wanajamii kwa kuwaongezea uwezo wa jinsi ya kuweza kukabiliana na matukio kama hayo kwa ustadi mkubwa katika kipindi kijacho.