SAMAKI AINA YA SILIKANTI AVULIWA BAHARI YA DAR ES SALAAM
Jumanne, 17 Julai 2024, Dar es Salaam
Samaki aina ya Silikanti amepatikana katika Soko la Samaki lililopo Feri jijini Dar es Salaam badaa ya kuvuliwa kimakosa katika eneo la Sinda Mnadani. Samaki huyo wa kale mwenye uzito wa kilo 87.7 na urefu wa sentimita 177 na hivyo kutoa mwono wa ajabu wa historia ya viumbe vya baharini.
Silikanti huyo atahifadhiwa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) katika Kitengo cha Shule ya Sayansi ya Madini na Teknolojia ya Uvuvi (SoAF) kwaajili ya vipimo na uchunguzi zaidi ikiwemo kipimo cha vinasaba (DNA). Silikanti mwenye jinsia ya kike amekutwa na jumla ya mayai ishirini na sita (26) katika tumbo lake.