'ROYAL TOUR' YAENDELEA KUTIKISA, WAGENI ZAIDI YA 200 WAFIKA KISIWA CHA SINDA
'ROYAL TOUR' YAENDELEA KUTIKISA, WAGENI ZAIDI YA 200 WAFIKA KISIWA CHA SINDA

 

Alhamisi, 28 Februari 2024, Dar es Salaam

Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu Tanzania (MPRU) imepokea Kundi la sita la watalii wa kigeni wapatao takribani 200 waliotoka ughaibuni kwa ajili ya kutembelea na kutalii ndani ya Eneo Tengefu la Kisiwa cha Sinda kilichopo katika Wilaya ya Kigamboni, Mkoa wa Dar es Salaam. 

Imetajwa watalii hao wametoka katika Nchi za Australia, Austria, Belgium, Canada, China, Ufaransa, Ujerumani, Poland, Urusi na Hispania huku wengine wakitokea Nchi za Switzerland, Uingereza na Marekani wakisafirishwa na Meli iitwayo "Le Bougainville" iliyokea Nchini Ufaransa. 

Akizungumzia ujio wa w ageni hao, Mhifadhi wa Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu, Bi. Catherine Msina alieleza kuwa wageni wamefurahishwa na vivutio vilivyopo Kisiwa hapo. 

 "Wamevutiwa na mbuyu ambao umefanana na umbo la shampeni lakini pia waneshukuru na kusema watakuja tena kutembelea kwani wamefurahia mandhari nzuri ambayo hawakuwahi kuiona sehemu zingine zote walizowahi kutembelea" alisema Msina.

Aidha, Vivutio vingine vinavyopatikana katika Kisiwa cha Sinda kama ni vile, 'German House’ Msitu wa Asili, Mapango, Matumbawe, Samaki wa aina tofauti tofauti kama Tuyuri (Crubs), Beach yenye Maji Ang'avu.