RAIS SAMIA AIKABIDHI TUZO HIFADHI ZA BAHARI NA MAENEO TENGEFU TANZANIA (MPRU)
Alhamisi, 29 Agosti 2024, Arusha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekabidhi tuzo kwa Taasisi ya Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu Tanzania (MPRU) mara baada ya Taasisi hiyo kushika nafasi ya Pili kati ya Taasisi 253 katika kipengele cha "Operational Excellence and Financial Performance"
Tuzo hiyo imepokelewa na Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Riziki Shemdoe akiwa sambamba na Kaimu Meneja wa MPRU, Bw. Davis Mpotwa.
Akizungumza mara baada ya kupokea tuzo hiyo Kaimu Meneja wa MPRU Bw. Davis Mpotwa alieleza kuwa tuzo hii itaenda kuongeza juhudi katika utendaji kazi wa taasisi na kuongeza chachu katika shughuli za uhifadhi wa bahari na utunzaji wa rasilimari zake ili kueleta tija kwa taifa kwa ujumla.
“Tuzo hii inaenda kutupa juhudi zaidi katika kuhakikisha kwamba tunaendelea kuboresha utendaji wetu lakini kuleta mafanikio katika taifa hili ili tupate kuwa na utendaji wenye tija kiujumla katika kuhakikisha kwamba maeneo ya Bahari yanahifadhiwa lakini pia vile viumbe ambavyo vinapatikana katika maeneo haya vinaendelea kuwepo kuhakikisha kwamba rasilimali zinakuwa endelevu” alisema Mpotwa.
Tuzo hiyo imetolewa Agosti 28,2024 katika Mkutano wa Wenyeviti wa Bodi na Wakuu wa Mashirika ya Umma na Taasisi za Serikali, Jijini Arusha.