WAZIRI MKUU MAJALIWA APONGEZA KUONGEZEKA IDADI YA WATALII KISIWANI MAFIA
WAZIRI MKUU MAJALIWA APONGEZA KUONGEZEKA IDADI YA WATALII KISIWANI MAFIA

Tarehe Iliyochapishwa: Jumamosi, Septemba 30,2023

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amepongeza kuongezeka kwa idadi ya watalii katika Kisiwa cha Mafia alipokuwa akihutubia katika sherehe za kufunga wiki ya uchumi wa bluu Kisiwa cha Mafia katika viwanja vya Mafia lodge, Utende.

“Ongezeko hili ni kubwa ,na ni matunda mazuri ya kampeni ya Rais Samia Suluhu Hassan katika Royal Tour, tumieni fursa hii tangazeni fursa zenu kupitia mifumo ya matangazo, na mchangamkie fursa za kufanya biashara” alisema Majaliwa. 

Alifafanua kwa kipindi Cha mwaka 2020/2023 Mafia imeongeza watalii na kufikia 14,153 na mapato yatokanayo na utalii Bilioni 2.7 ,na kusema hili ni ongezeko kubwa.

Aliupongeza mkoa na wilaya kwa kufanikisha tamasha hilo na kutangaza vivutio vya Mafia na kuwashauri lisiishie hewani liwe endelevu kwa kila mwezi septemba ya kila mwaka.

Majaliwa alieleza, Mafia ni kisiwa ambacho kinasifika kwa mazalia ya samaki Duniani, kisiwa hiki kinachangia pato kubwa kupitia Uchumi wa bluu na uvuvi.