MPRU YASHIRIKI ZIARA YA MAFUNZO NCHINI MSUMBIJI
MPRU YASHIRIKI ZIARA YA MAFUNZO NCHINI MSUMBIJI

Jumatatu, 04 Novemba 2024, Msumbiji

Hifadhi ya Bahari na Maeneo Tengefu Tanzania (MPRU) imeshiriki ziara ya mafunzo katika Kisiwa cha Bazaruto kilichopo ndani ya Hifadhi ya Kitaifa ya Barazuto Archipelago nchini Msumbiji.

Katika ziara hiyo, Mhifadhi Mfawidhi kutoka MPRU, Bi. Maria Pentzel ambaye aliambatana na Mhifadhi kutoka Hifadhi Bahari ya Kisiwa cha Mafia (MIMP) Bernard Ngatunga waliiwakilisha MPRU katika ziara hiyo iliyolenga kuwezesha kubadilishana maarifa kuhusu mbinu bora katika Usimamizi wa Maeneo yaliyohifadhiwa ya Bahari (MPAs), ushirikishwaji wa jamii, maisha mbadala, na mifumo endelevu ya uhifadhi.

Ziara hiyo iliyoungwa mkono na Heshimu Baharii chini ya Shirika la misaada la Kimataifa la USAID unaolenga kuboresha usimamizi wa Maeneo yaliyohifadhiwa ya Bahari (MPAs) nchini Tanzania. Archipelago la Bazaruto linatumika kama mfano mzuri kutokana na mikakati yake ya usimamizi wa pamoja ambayo imepelekea kuboreshwa kwa afya ya ikolojia na ustawi wa jamii.

Kupitia ushiriki wa MPRU katika ziara hii ya masomo huko Bazaruto inatarajia kujifunza mifumo sawa ya usimamizi wa pamoja inayosisitiza kujenga uwezo miongoni mwa wafanyakazi kama vile programu za mafunzo kwa walinzi na wafanyakazi ofisini.

Tanzania inaweza kuongeza ufanisi wa MPAs zake kama kipaumbele kwenye fursa za ajira zinazojumuisha jinsia ndani ya mifumo hii pia kutawezesha ushiriki tofauti katika juhudi za uhifadhi.