MPRU YASHIRIKI WARSHA KUJADILI MAENDELEO YA UTALII MAENEO YA PEMBEZONI MWA BAHARI YA HIND
MPRU YASHIRIKI WARSHA KUJADILI MAENDELEO YA UTALII MAENEO YA PEMBEZONI MWA BAHARI YA HIND

Jumamosi, 16 Novemba, 2024, Dar es Salaam

Hifadhi ya Bahari na Maeneo Tengefu Tanzania (MPRU) imeshiriki warsha ya kujadili maendeleo ya utalii katika maeneo ya pembezoni mwa Bahari ya Hindi (Coastal Tourism Development). 

Warsha hiyo ilifunguliwa rasmi Novemba 14-15, 2024 katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Utalii kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Bw. Philip Chitaunga kwa niaba ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Pindi Chana 

Aidha, warsha hiyo ilidumu kwa muda wa siku mbili Novemba 14-15, 2024 ilifungwa rasmi na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Edwin Mhede kwa niaba ya  Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega.

Kwa upande wake, Kaimu Meneja wa Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU), Bw. Davis Mpotwa aliongoza uwakilishi wa MPRU katika hafla hiyo akiongoza mijadala, maswali na majibu.