MPRU YASHIRIKI HAFLA YA MAKABIDHIANO YA VIFAA VITAKAVYOTUMIKA KATIKA SHUGHULI ZA UHIFADHI
MPRU YASHIRIKI HAFLA YA MAKABIDHIANO YA VIFAA VITAKAVYOTUMIKA KATIKA SHUGHULI ZA UHIFADHI

Jumanne, 15 Octoba 2024, Tanga

Kaimu Meneja wa Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU), Bw. Davis Mpotwa (wapili kulia) ameshiriki katika hafla fupi ya makabidhiano ya vifaa kwa ajili ya shughuli za Uhifadhi (Urejeshaji wa matumbawe) katika Hifadhi ya Bahari ya Silikanti-Tanga.

Katika hafla hiyo ya makabidhiano ya vifaa hivyo kupitia udhamini wa Shirika lisilo la kiserikali la Jumuiya ya Uhifadhi wa Wanyamapori (WCS), vifaa vilivyokabidhiwa ni jengo la kwaajilili ya kutunzia vifaa vya uzamiaji, boti na injini yake zitatumika katika shughuli za urejeshaji wa Matumbawe (Coral Reef Restoration) pamoja na pikipiki mbili (2) aina ya Yamaha.

Vifaa vyote vilivyokabidhiwa vitatumika uendeshaji wa shughuli za Mradi wa Blue Action Fund II (BAF)  kwa awamu ya pili ili kutekeleza shughuli za urejeshaji wa Bioanuwai na kupambana na Mabadiliko ya Tabia nchi.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na watumishi wa Hifadhi za Bahari ya Tanga Silikanti (TACMP), Maafisa mbalimbali wa Serikali katika ngazi ya Wilaya (Muheza na Jiji), Mkoa na uwakilishi kutoka Ofisi za Wizarani Tanga pamoja na timu kutoka WCS tarehe 15.10.2024 katika eneo la Ofisi ya TACMP iliyopo kata ya Kigombe jijini Tanga.