MPRU YAFANYA KIKAO NA KAMATI YA USALAMA YA MKOA WA LINDI
MPRU YAFANYA KIKAO NA KAMATI YA USALAMA YA MKOA WA LINDI

Jumanne, Januari 14, 2025 Lindi

Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU) imefanya kikao kazi zna Kamati ya Usalama ya Mkoa wa Kilwa ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack.

Kikao hicho kilichofanyika Januari 09, 2025 katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi kiliwakutanisha Timu ya Wataalam kutoka MPRU ikiongozwa na Mhifadhi Mkuu Bw. Godfrey Ngupula na Kamati ya Usalama ya Mkoa wa Lindi.

Kikao hicho kilibeba dhima ya kuhifadhi visiwa vilivyopo katika Wilaya ya Kilwa ikiwemo Eneo Tengefu la Kilwa na kuilinda ‘Gulf of Kilwa’ na vivutio vyake ikiwemo Hifadhi ya Bahari ya Kilwa.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack alifurahia kusikia lengo la MPRU katika kuhifadhi vivutio vilivyopo katika Wilaya hiyo na kuwataka wafanikishe kwa haraka zoezi hilo ikiwezekana kabla ya uzinduzi wa Bandari ya Uvuvi Kilwa uliyofikia zaidi ya 80% mpaka kukamilika kwake ambapo inatarajiwa kuzinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.