MPRU YAENDESHA PROGRAMU YA MAFUNZO KWA WANAFUNZI UDSM

Alhamisi, Februari 13, 2025, Dar es Salaam
Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu Tanzania imeendesha programu ya mafunzo kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ili kuweza kufahamu na kujifunza shughuli mbalimbali zinazofanywa na MPRU.
Mafunzo hayo yaliyoanza kuanzia Februari 6-12, 2025, yakiongozwa na Afisa Masoko wa MPRU, Halima Tosiri akishirikiana na Afisa Uhusiano, Bw. Ivan Kimaro yalifanyika kwa mafaniko makubwa kwa kushuhudia idadi kubwa ya wanafunzi kutembelea Banda la MPRU lililopo katika viwanja vya chuo hicho kufahamu na kujifunza shughuli zinazofanywa na taasisi hiyo.
Wanafunzi hao walioweza kufika katika Banda la MPRU walipata fursa ya kujifunza kuhusiana na Utalii wa Bahari na shughuli za Uhifadhi wa Rasilimali za Bahari zinavyoendeshwa ikiwa ni hatua moja wapo ya kuendana na sera ya Uchumi wa Buluu kuhakikisha inakua kupitia rasilimali zetu za Bahari tulizonazo nchini.
Aidha, naye Afisa Utalii wa Dar es Salaam Marine Reserves System (DMRS), Bw. Sifuni Sospatery alishiriki kikamilifu katika programu hiyo ya utoaji wa elimu kwa wanafunzi hao wa Chuo cha UDSM.