MPRU YASHIRIKI KONGAMANO LA 14 LA MWAKA LA WATAALAM WA UNUNZI NA UGAVI
MPRU YASHIRIKI KONGAMANO LA 14 LA MWAKA LA WATAALAM WA UNUNZI NA UGAVI

Tarehe Iliyochapishwa: Jumatatu, Desemba 18, 2023

Maafisa Ugavi na Manunuzi kutoka Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu Tanzania (MPRU) wameshiriki katika Ufunguzi wa Kongamano la 14 la Mwaka la Wataalam wa Ununuzi na Ugavi lililofanyika katika Ukumbi wa Simba katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC).

Aidha, Serikali imewaagiza waajiri wa Sekta zote nchini kuhakikisha wataalam wanaofanya shughuli za ununuzi na ugavi wanakuwa na sifa sitahiki kama ilivyoainishwa kwenye Sheria Na. 23 ya mwaka 2007 iliyoanzisha Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), pamoja na miongozo inayotolewa.

Maagizo hayo yametolewa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), wakati akifungua Kongamano la 14 la Wataalam wa Ununuzi na Ugavi.

Maafisa hao wa Ununuzi walioshirki mkutano huo ni Bw. Richard Mwakisisya, Bw. John Mweluwe pamoja na Bw. Suleiman Mohamed.