MPRU, NM-AIST & TAFIRI WAFANYA KIKAO KUJADILI MFUMO WA UKUSANYAJI WA TAARIFA ‘PHOTOQUADRAT
Jumatano, 14 Februari 2024, Dar es Salaam
Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu Tanzania (MPRU) na Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) kwa kushirikiana na Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) imefanya kikao cha uwezeshaji wa utumiaji wa mfumo wa ukusanyaji wa taarifa katika maeneo ya Uhifadhi kwa kutumia picha ujulikanao kama ‘Photoquadrat’ .
Meneja Mteule (MPRU) Bw. Davis Mpotwa kwa kushirikiana na Mhifadhi Mkuu Bw. Godfrey Ngupula aliongoza kikao hicho ambapo pia kilihudhuriwa pia na watumishi pamoja na wale wa vituoni walioshiriki kupitia Njia ya Mtandao.
Wataalam, Bw. Masumbuko Semba (NM-AIST) na George Rushingisha (TAFIRI) waliongoza uelekezaji wa mfumo huo wa ukusanyaji taarifa kupitia picha ‘Photoquadrat’.