MPRU, GIZ WAKUTANA KUFANYA MAJADILIANO MRADI WA TRANSBOUNDARY CONSERVATION AND SUSTAINABLE USE OF COST AND MARINE BIODIVERSITY
MPRU, GIZ WAKUTANA KUFANYA MAJADILIANO MRADI WA TRANSBOUNDARY CONSERVATION AND SUSTAINABLE USE OF COST AND MARINE BIODIVERSITY

Jumanne, 30 Aprili 2024, Dar es Salaam

Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu Tanzania (MPRU) imekutana na wawakilishi kutoka Shirika la Deutsche Gesellschaft fὒr Internationale Zusammenarbeit (GIZ) na kufanya majadliano juu ya utekelezaji wa mradi ujulikanao kama “Transboundary Conservation and Sustainable use of Cost and Marine Biodiversity”. 

Mradi huo unaotarajia kuanza hivi karibuni ukishirikisha nchi za Tanzania na Kenya, ambapo kwa upande wa Kenya mradi huu utatekelezwa katika eneo la Kwale na hapa Tanzania mradi huo utajumuisha katika eneo la Hifadhi ya Silikanti lililopo mkoa wa Tanga. 

Mradi huu wa GIZ utajihusisha utunzwaji wa rasilimali za bahari kwa maeneo ya hifadhi na pembezoni mwa bahari katika mkoa wa Tanga. Kwa kushirikisha jamii ya Pwani pamoja na maeneo yote mradi.

MPRU inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya uhifadhi na matumizi endelevu ya rasilimali za bahari yanayochochea ukuaji wa uchumi wa Buluu, ikiwemo mradi unaoendelea wa uokoaji wa matumbawe (Coral Reef Rescue Project) ambao unalenga kuhakikisha utunzwaji wa miamba ya matumbawe. Matumbawe ni rasilimali muhimu baharini ikiwa ni vivutio, makazi na mazalia ya aina mbalimbali ya viumbe wanaopatikana baharini. 

MPRU inatoa ushirikiano na kuhamasisha mashirika mbalimbali pamoja na wadau wanaojihusisha na shughuli za uhifadhi wa bahari katika utekelezaji wa miradi ya uhifadhi ili kuwezesha uwepo na matumizi endelevu ya rasiliamali mbalimbali zinazopatikana baharini kwani ni nyenzo muhimu ya maendeleo ya uchumi wa Buluu nchini.