MKUU WA WILAYA TANGA MJINI ATEMBELEA VISIWA VYA YOMBE, ULENGE, TOTENI
MKUU WA WILAYA TANGA MJINI ATEMBELEA VISIWA VYA YOMBE, ULENGE, TOTENI

Jumanne, 12 Novemba 2024, Tanga

Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mhe. Japhari Kubecha amefanya ziara ya kutembelea visiwa vilivyopo ndani ya Wilaya ya Tanga Mjini ikiwemo Visiwa vya Yambe, Ulenge, Toteni pamoja na Fungu la Mchanga ijulikanalo kama Nyuli vinavyopatikana katika Mkoa wa Tanga.

Katika ziara yake hiyo iliyofanyika Novemba 11, 2024,  Mhe. Kubecha aliambatana na Maafisa kutoka Hifadhi ya Bahari ya Tanga Silikanti (TACMP) akiwemo Afisa Utalii Bw. Jamal Mvungi pamoja na Afisa Mazingira kutoka Halmashauri ya jiji la Tanga Mjini Bi. Zamoyoni Mohamed.

Aidha, akiwa katika ziara hiyo Mhe. Kubecha  alipongeza jitihada na kazi nzuri  za shughuli za uhifadhi zinazofanywa katika kuhifadhi visiwa hivyo pamoja na ulinzi madhubuti na kuyataka maeneo hayo ya visiwa kuongezewa nguvu hususan kwenye masuala ya utalii kwa kuyaainisha na kutangaza kwajili ya fursa nzuri ya uwekezaji katika visiwa hivyo.

Halikadhalika, aliongeza kuwa atakuwa mstari wa mbele katika juhudi za kutafuta wawekezaji watakaoweza kuwekeza katika visiwa hivyo itakayopelekea kujitangaza na kuinua utalii wa ndani hasa utalii wa bahari.