MKURUGENZI WA UTAFITI NA MAFUNZO WIZARA YA MALIASILI NA UTALII ATEMBELEA BANDA LA MPRU
MKURUGENZI WA UTAFITI NA MAFUNZO WIZARA YA MALIASILI NA UTALII ATEMBELEA BANDA LA MPRU

Jumamosi, 10 Agosti 2024, Dodoma

Kaimu Meneja Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU) Bw. Davis Mpotwa (kulia) akutana na Mkurugenzi wa Utafiti na Mafunzo Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Edward Kohi na kujadili masuala mbalimbali yanayohusu Utalii wa maeneo ya Bahari.
Miongoni mwa yaliojadiliwa ni pamoja na uboreshwaji wa takiwimu za kitalii na kitafiti katika Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu, kuongeza juhudi za kujitangaza kitaifa na kimataifa sambamba na kutumia miradi kuboresha miundombinu ya utalii katika Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu.


Kwa upande wake, Mkurugenzi wa  Utafiti na Mafunzo Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Kohi amesema lengo la Taifa ni kuboresha mazingira ya kuwavutia watalii na kufungua maeneo kwa ajili ya utalii.
Kwa upande wake Kaimu Meneja Bw. Mpotwa amemshukuru Mkurugenzi huyo kwa ushirikiano na mikatati ya kuongeza wigo wa utalii wa Bahari, ikiwa ni juhudi madhubuti za kuunga mkono jitihada za kuongeza pato la taifa kupitia uchumi wa buluu hususan upande wa utalii hapa nchini Tanzania.