MKURUGENZI MSAIDIZI WIZARA YA UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO APONGEZA TAMASHA LA MAFIA FESTIVAL 2024
MKURUGENZI MSAIDIZI WIZARA YA UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO APONGEZA TAMASHA LA MAFIA FESTIVAL 2024

Jumanne, Disemba 17 2024, Mafia

Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo Sanaa kutoka Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Asha Salim ameipongeza Wilaya ya Mafia kwa kuandaa Tamasha la Mafia Festival 2024 huku akielezea mchango wake katika kukuza utalii na utamaduni Kisiwani Mafia na Taifa kwa ujumla.

Dkt. Asha Salim aliyasema hayo Disemba 07, 2024 alipokuwa akihutubia katika viwanja vya Utende vilvyopo katika Wilaya ya Mafia mkoa wa Pwani.

"Matamasha kama haya ni muhimu sana katika kuendeleza, kuibua utamaduni wetu wa manzanita ikiwemo sanaa" alisema Dkt. Asha.

Viongozi kutoka taasisi mbalimbali za Kiserikali na zisizo za serikali, wafanyabiashara, wadau wa utalii pamoja wananchi kwa ujumla walijitokeza kushiriki tamasha hilo na kutembelea mabanda ya maonesho kuona bidhaa na huduma zitolewazo na wadau wa utalii, uhifadhi wa mazingira na wafanyabiashara kwa ujumla, hususan katika masuala ya Uchumi wa Buluu.

Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU) ilishirki katika Tamasha hilo kama wahifadhi wa  wa Bahari huku ikiweza kuonesha huduma zake kwa wageni waliopata nafasi ya kufika katika banda lake la maonesho.

Aidha, Kauli mbiu kwa mwaka huu katika Tamasha hili la utalii (Mafia Festival 2024) ilikuwa ni “ Wekeza katika uchumi wa buluu Kisiwani Mafia”.