MKURUGENZI MKUU BAHARI NA UVUVI TUME YA UMOJA WA NCHI ZA ULAYA ATEMBELEA KISIWA CHA MBUDYA
Jumanne, 10 Septemba 2024, Dar es Salaam
Mkurugenzi Mkuu wa Masuala ya Bahari na Uvuvi kutoka Umoja wa Nchi za Ulaya, Bi. Charlina Vitcheva ametembelea Kisiwa cha Mbudya akiwa ameambatana na wenzake mara baada ya kuwasili nchini katika ziara rasmi.
Bi. Charlina Vitcheva aliambatana na mwenyeji wake Bw. Davis Mpotwa, Kaimu Meneja wa Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu Tanzania (MPRU) katika matembezi ndani ya Kisiwa hicho cha Mbudya.
Halikadhalika, katika msafara huo Bi. Charlina Vitcheva aliongozana na wageni pamoja na viongozi wengine mbalimbali akiwemo Mkurugenzi wa Uvuvi, Prof. Mohamed Sheikh, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI), Dkt. Ismael A. Kimirei.
Aidha, Bi. Charlina ameipongeza Taasisi ya Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu Tanzania (MPRU) kwa juhudi zao thabiti za uhifadhi.
Umoja wa Ulaya inaendelea kusaidia mtandao wa Maeneo ya Hifadhi ya Bahari (MPAs) wa Tanzania kulinda viumbe hai wa baharini na kupambana mabadiliko ya tabianchi.