MAENEO MAALUM ‘CRITICAL HABITATS’ YATAKIWA KULINDWA ILI KULETA UHAI WA BAHARI
MAENEO MAALUM ‘CRITICAL HABITATS’ YATAKIWA KULINDWA ILI KULETA UHAI WA BAHARI

Jumatano, Machi 05, 2025, Dar es Salaam.

Mhifadhi Mkuu kutoka Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu Tanzania (MPRU), Bw. Godfrey Ngupula ameeleza kuwa maeneo maalum ‘critical habitats’ yanatakiwa kulindwa ili kuleta uhai wa Bahari.

Bw. Ngupula aliyasema hayo alipokuwa akihojiwa na Kituo cha habari cha Clouds TV katika kipindi cha Sentro na kueleza kuwa maeneo hayo maalum ni muhimu katika ulinzi hai wa Bahari. 

“Bahari ili iweze kuwa hai ikupe hichi ambacho inakupa leo kule kuna maeneo maalum ambayo yapo tunayaita critical habitats ndani ya bahari tunayatambua mfano kwa urahisi sana ili bahari iweze kuendelea kuwepo hivi ina maeneo ambayo ni ya mazalia ya viumbe wa baharini, maeneo ambayo ni maficho ya viumbe wa baharini kwasababu kuna maadui wapo kwa mfano samaki wanakulana kwa wenyewe, alisema Ngupula.

Sasa ili mavuvi yaendelee na samaki waendelee kuwepo kuna hayo maeneo ambayo ni maficho, makuzi na malazi ya baharini lakini kuna maeneo ambayo pia ni vyakula na ni maalumu kwaajili ya kukua yakiwepo kwa wingi ni vizuri sana yalindwe ili kuweza kuleta huo uhai wa bahari” aliongezea Bw. Ngupula. 

Aidha, Afisa Utalii Bw. Sifuni Sospatery naye alishiriki katika mahojiano hayo na kuhimiza watalii wa ndani na nje ya nchi kutembelea Hifadhi za Bahari kujionea utalii uliopo katika Bahari.