FUKWE NZURI, MATUMBAWE NI MOJA YA VIVUTIO VIKUBWA KATIKA KISIWA CHA SINDA
Ijumaa, 26 Aprili 2024, Dar es Salaam
Mhifadhi Bahari kutoka Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu Tanzania Bi. Catherine Msina ameweka wazi kuwa uwepo wa fukwe safi pamoja matumbawe ni katika Kisiwa cha Sinda ndio chanzo kikubwa kinachowavutia watalii kuja kutembelea katika Kisiwa hicho.
Bi. Msina ameyasema hayo mara baada ya ujio ya Meli kubwa ya kitalii ya kigeni ijulikanayo kama “Silver Cloud” iliyobeba watalii zaidi ya 200 kutia nanga katika Hifadhi za Bahari ya Kisiwa cha Sinda.
“Hii inapeleka ujumbe kwamba sisi kutokana na uhifadhi wetu wa maeneo haya ya Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu inaonekana sasa tumeanza kutambulika na wanavutiwa na maeneo yetu yaliyokuwepo hapa yana fukwe nzuri ambayo mtu anaweza kuogelea na akainjoi lakini matumbawe yaliyokuwepo” alisema Msina.
Aidha, Bi. Msina alieleza kuwa haya ni matokeo chanya ya Filamu ya “The Royal Tour” iliongozwa na Rais Samia kuweza kufungua milango kwa watalii wengi kuja kutembelea vivutio mbalimbali vinavyopatikana nchini.
“Nimefurahia vivutio vilivyopo katika Kisiwa hiki cha Sinda ina fukwe nzuri na upepo tulivu pia mandhari nzuri ambayo ukikaa hapa unaweza kuona jiji la Dar es Salaam kwa ukubwa wake” alisema George Burton, Mtalii kutoka wa Uingereza.