WATAALAM KUTOKA OFISI YA MAKAMU WA RAIS WATEMBELEA KISIWA CHA MAFIA
WATAALAM KUTOKA OFISI YA MAKAMU WA RAIS WATEMBELEA KISIWA CHA MAFIA

Jumatatu, 18 Machi 2024, Mafia

Timu ya Hifadhi ya Bahari ya Kisiwa cha Mafia (MIMP) imepokea ugeni wa Wataalam kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais ambapo wamekuja kujionea fursa zinazopatikana katika Kisiwa hicho ikiwa ni katika kuhimiza dhana ya Uchumi wa Buluu (Blue Economy) nchini pamoja na kuhamasisha Uhifadhi wa Mazingira.

Wataalam hao pia wapo katika maandalizi ya kuandaa Makala (Documentary) wamefika kujionea fursa pamoja na shughuli nzima zinazofanywa Kisiwani huko katika ukanda wa Pwani ikiwa ni pamoja na Ukulima wa Mwani katika Kisiwa cha Jibando.

Halikadhalika, waliwatembelea mpaka kwa Wavuvi wanaojishughulisha na uanikaji dagaa, pamoja na kujionea Kisiwa cha Shungimbili chenye vivutio vya asili kama Matumbawe (Corals Reefs), Nyasi Bahari (Sea grass) na vivutio vingine vinavyopatikana katika Kisiwa hicho.