Viongozi Uhifadhi wakutana na Mkuu wa USAID
Tarehe Iliyochapishwa: Ijumaa, Juni 23, 2023
Mkuu wa Shirika la Misaada la Kimarekani (USAID) Balozi Samantha Power amekutana na Viongozi wanawake wa Uhifadhi ambao wanashirikiana na shiriki la hilo la misaada na viongozi hao kupata fursa ya kuelezea jinsi shughuli za uhifadhi zinavyofanyika, kikao hicho kimefanyika jijini Arusha. Katika majadiliano Viongozi hao wanawake wa Uhifadhi nchini kutoka serikalini na taasisi zisizo za kiserikali walielezea namna wanafanya kazi kwa pamoja kuhakikisha jumuiya za ndani zinanufaika kupitia juhudi za uhifadhi kama vile uvuvi endelevu , uhifadhi wa misitu kupitia “carbon credits” na utalii wa wanyama pori. Meneja wa MPRU, Dkt. Immaculate Sware Semesi wa nne kutoka kulia(pichani) pamoja na viongozi wengine wa uhifadhi wakiwa katika picha ya pamoja na Balozi Samantha mara baada ya kumaliza kwa hicho.