MKUTANO WA WA MABADILIKO YA TABIA NCHI NA NAMNA YA KUZUIA ATHARI KATIKA MAENEO TENGEFU
Tarehe Iliyochapishwa: Ijumaa, Disemba 08, 2023
Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu Tanzania itashiriki katika mkutano wa Kimataifa wa Mabadiliko ya Tabia Nchi (COP28) katika mji wa Dubai, UAE. Mkutano huo ambao unalenga katika kuhakikisha kunakuwepo na mpango mkakati wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi pamoja na athari zake.
Aidha, Mhifadhi wa Bahari kutoka Hifadhi za Bahari ya Kisiwa cha Mafia (MIMP) Bw. Ailars David kwa upande wake alipata nafasi ya kushiriki mahojiano hayo ya juu kuhusu Maeneo Tengefu na mchango wake katika kukabiliana na mabadiliko ya Tabia Nchi pamoja na azimio la 30x30 ambapo mahojiano hayo yalioandaliwa na Shirika la 'Times for the Better'.
Halikadhalika, Bw. Ailars ameeleza namna MPRU kama Taasisi ya Serikali inavyendesha shughuli za Ulinzi wa Uhifadhi wa Baharini (MPAs) nchini lilivyo jipanga kuhakikisha tunakubaliana na mabadiliko ya Tabia Nchi kama vile kuongeza shughuli za urejeshaji ikijumuisha upandaji wa Mikoko, Matumbawe na Nyasi Bahari.
Bw. Ailars aliongezea kwa kuomba ushirikiano na sapoti kutoka kwa wadau katika kufanikisha hili swala kwa pamoja.