AFO YAISHIRIKISHA MBREMP MAFUNZO YA UZAMIAJI 'TANZANIA DIVE LAB 2024'.
AFO YAISHIRIKISHA MBREMP  MAFUNZO YA UZAMIAJI 'TANZANIA DIVE LAB 2024'.

Jumatatu, 12 Agosti 2024, Mtwara.

Shirika la Aqua-Farms Organization (AFO) imeishirikisha Hifadhi ya Bahari ya Ghuba ya Mnazi na Maingilio ya Mto Ruvuma (MBREMP) katika kuzindua programu ya mafunzo ya kupiga mbizi ijulikanao kama Tanzania Dive Lab 2024 inayofanyika ndani ya kituo cha MBREMP kilichopo Mkoani Mtwara.

Mpango huu unalenga kukuza ujuzi wa kuzamia  kwa wafanyakazi kiwango cha 'Dive Masters'  idadi ya wafafanyakazi sita (6) na kiwango cha 'Open Water' kwa idadi zaidi ya ishirni (20).

MPRU kupitia kituo cha MBREMP imepewa nafasi 5 za wafanyakazi na wanajamii ambao watapatiwa mafunzo hayo. Mwisho wa mafunzo hayo matarajio ni kuwa yataongeza kwa kiasi kikubwa uwezo wa utafiti na ufuatiliaji wa rasilimali za baharini pamoja na kuimarisha juhudi za uhifadhi na tija.