WADAU WAKUTANA KUTATHIMINI MRADI WA USIMAMIZI WA RASILIMALI ZA BAHARI
WADAU WAKUTANA KUTATHIMINI MRADI WA USIMAMIZI WA RASILIMALI ZA BAHARI

Tarehe Iliyochapishwa: Alhamisi, Octoba 05, 2023

Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu nchini kwa kushirikiana na Kamati tendaji ya mradi wa ushirikiano kati ya Nairobi Convention na Southwest Indian Ocean Commission imekutana kwa ajili ya kufanya tathmini ya mradi huo unaolenga usimamizi wa mazingira ya bahari na nchi kavu pamoja na usimamizi wa rasilimali za uvuvi kilichofanyika kwenye ukumbi wa chuo cha VETA Mkoani Tanga.

 Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI ), Dkt. Ismael Kimirei amebainisha hayo Oktoba 04,2023 ambapo amesema kuwa mradi huo unaotekelezwa katika Wilaya ya Mkinga na Pemba unalenga kutoa majibu ya mahitaji katika uchumi wa buluu.

"Tumeanzia eneo la Mkinga kwa sababu huu ni mradi wa ushirikiano kati ya Tanzania, Msumbiji na Madagascar na tunategemea kwamba utapanuka kwenda nchi nyingine na ukiangalia upande wa kaskazini mwa bahari ya Hindi kuna nchi ya Kenya ambayo tunatarajia iwe mdau katika mradi huu"  alisema Bi Oliver.

Kwa upande wake, Mratibu wa Mradi unaoshughulikia maendeleo ya usimamizi wa rasilimali za bahari kutoka Shirika la Chakula na kilimo (FAO) Bi. Oliver Mkumbo amesema kuwa mradi huo unathamani ya dola za marekani milioni 8 ambazo zimegawanywa katika nchi tatu.

"Kubwa ni kuangalia namna gani tuboreshe mazingira lakini wakati huo huo kuangalia rasilimali zilizopo ukanda wa Pwani zimekuwa endelevu na maisha ya watu yameboreshwa kwa shughuli zinazofanyika.

Katika picha hapo juu ni wadau akiwemo Meneja wa Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu nchini Dkt. Immaculate Sware Semesi baada ya kikao cha kamati tendaji cha mradi wa ushirikiano wa SWIOFIC Nairobi Convention.