MWAMPOSA, SHEIKH. WALID MABALOZI WAPYA WA UHIFADHI WA BAHARI- WAZIRI ULEGA.
MWAMPOSA, SHEIKH. WALID MABALOZI WAPYA WA UHIFADHI WA BAHARI- WAZIRI ULEGA.

Tarehe Iliyochapishwa: Ijumaa, Juni 16, 2023

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega amesema Wizara yake itawatumia Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Shekhe Walid Alhad Omar na Mchungaji wa Kanisa la Arise and Shine na Boniface Mwamposa kuwa mabalozi wa uhifadhi wa Bahari ili wasaidiane nao katika kuelimisha jamii hasa zinazoishi kando ya Bahari juu ya athari ya uvuvi haramu na uharibifu wa mazingira ya Bahari kwa ujumla.

Waziri Ulega alisema hayo wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Bahari Duniani yaliyofanyika jijini Dar es Salaam Juni 8, 2023.

Alifafanua kuwa pamoja na uwepo wa Sheria kwenye usimamizi na uendelevu wa rasilimali za Bahari, ni muhimu pia kushirikiana na jamii katika kuhakikisha mazingira ya Bahari yanahifadhiwa vizuri kwa maslahi ya mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

Alisema kwa kutambua umuhimu wa kushirikisha jamii wameamua kuwatumia Viongozi hao wa Dini kuwa mabalozi na kuwaelimisha juu ya umuhimu wa kuepuka vitendo ambavyo vinapelekea uharibifu wa mazingira ya Bahari.

"Sisi Wizara na Kitengo chetu cha MPRU tupo tayari kushirikiana na viongozi hawa ili waweze kutusaidia kutoa elimu kwa jamii juu ya athari ya Uvuvi haramu na uharibifu wa mazingira", aliongezea Mhe. Ulega.