MPRU YASHIRIKI PROGRAMU YA MAFUNZO YA MSP KWA NCHI ZA UKANDA WA PWANI YA MAGHARIBI YA BAHARI YA HINDI
MPRU YASHIRIKI PROGRAMU YA MAFUNZO YA MSP KWA NCHI ZA UKANDA WA PWANI YA MAGHARIBI YA BAHARI YA HINDI

Tarehe Iliyochapishwa: Jumatatu, Octoba 16, 2023

Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu kupitia imeshiriki programu ya mafunzo ya mpango wa matumizi wa maeneo ya bahari (MSP) kwa nchi za ukanda wa Pwani ya Magharibi ya Bahari ya Hindi uliofanyika kwa njia ya mtandao octoba 11, 2023.

Mhifadhi kutoka Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu Tanzania Bi. Maria Pentzel ambaye alikuwa akiwakilisha kwa upande wa MPRU katika kuchangia na kuelezea masuala mazima ya uhifadhi wa bahari alikuwa miongoni mwa washiriki wataalam walioteuliwa kujiunga na mpango huo wa mafunzo kutoka Tanzania Bara pamoja na wataalam wengine kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo. ,  na Shule ya Upili ya Sayansi ya Acqua na Teknolojia ya Uvuvi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Aidha, Sektratieti ya Mkataba wa Nairobi kuhusu Uhifadhi, Usimamizi na Uendelezaji wa Mazingira ya Ukanda wa Pwani ya Magharibi ya Bahari ya Hindi iliingia makubaliano na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la nchi ya Swedeni (The Swedish International Development Cooperation Agency – SIDA) kwa ajili ya kuendesha mafunzo kuhusu mpango wa matumizi wa maeneo ya Bahari (MSP) katika nchi za ukanda wa Pwani ya Magharibi ya Bahari ya Hindi ambazo ni wanachama wa Mkataba wa Nairobi.

 Makubaliano hayo yametokana na uhitaji wa nchi wanachama wa mkataba wa Nairobi kupata mafunzo na kujengewa uwezo kuhusu MSP katika nchi zimeonesha uhitaji wa kupata mafunzo hayo ni pamoja na Tanzania, Kenya, Msumbiji, Somalia, Madagascar, Mauritius na Comoro. Aidha, nchi ya Afrika Kusini na Seychelles hazipo katika mafunzo hayo kwakuwa tayari zimepiga hatua katika kuandaa mpango huo.

Halikadhalika, ili kufanikisha mafunzo haya kwa njia ya ITP, Taasisi ya SwAM imeingia makubaliano na Kampuni ya NIRAS kwa ajili ya kuendesha mafunzo hayo kwa njia ya (International Training Program – ITP) kwa nchi husika.   Kampuni hii hutoa huduma mbalimbali ikiwemo huduma ya utaalamu elekezi na mafunzo. Kampuni ya NIRAS imekuwa na uzoefu wa kufanya mafunzo mbalimbali kwa njia ya Program ya Mafunzo ya Kimataifa (International Training Program-  ITP). 

Hivyo, kampuni hii inasaidia Taasisi ya SwAM kwa kutoa utaalam elekezi katika kufanikisha malengo ya mafunzo haya. Lengo la Programu ni kuimarisha uwezo wa wataalam na Taasisi katika kuanzisha, kuandaa na kutekeleza MSP katika nchi zao.

.