WATUMISHI MPRU WAPATIWA MAFUNZO YA MFUMO WA NeST
WATUMISHI MPRU WAPATIWA MAFUNZO YA MFUMO WA NeST

Tarehe Iliyochapishwa: Jumamosi, Octoba 21, 2023

Mtendaji Mkuu wa Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu nchini Dkt. Immaculate Sware Semesi amefanya kikao na washiriki wa mafunzo ya mfumo mpya wa manunuzi (NeST) na kujadiliana jinsi mfumo huo utakavyofanya kazi na kueta tija ambapo kikao hicho kilichofanyika katika Makao Makuu ya ofisi za MPRU zilizopo Upanga jijini Dar es Salaam. 

NeST ni Mfumo mpya wa kielektroniki wa manunuzi ya Umma yaani National - e - Procurement System, mfumo ambao umeundwa na wazawa hapa nchini. Mfumo huo unaotarajiwa kuwa mbadala wa mfumo wa awali wa manunuzi ya Umma uliojulikana kama Tanzania National e Procurement System yaani TANePS.

Mwishoni Julai 31 hadi Agosti 4 mwaka huu, Serikali kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa ununuzi wa Umma – PPRA, ilianza rasmi kutoa mafunzo ya kwa wataalamu ngazi ya mikoa namna ya kutumia mfumo wa NeST, wataalamu sita kwa kila Mkoa wa Tanzania Bara. 

Mfumo huu wa NeST umeundwa na wazawa wenyewe kuna uhakika wa asilimia kubwa mfumo utaongeza usiri na usalama kwa nyaraka za Serikali ukilinganisha na mfumo wa TANeMPS uliokuwa chini ya wageni.

Aidha,  mfumo wa wazi kwa kuwa kila mchakato wa manunuzi ya Umma utakaofanyika ndani ya mfumo, kila aliyepewa dhamana ya kuingia kwenye mfumo huo atakuwa anaona au kujua kinachoendelea humo hivyo kupunguza changamoto ya rushwa wakati wa mchakato wa kutangaza zabuni.

Katika picha ni Washiriki wa Mafunzo ya Mfumo mpya wa Manunuzi NeST wa MPRU wakiwa na Mtendaji Mkuu wa MPRU.