MLIBWENDE WA DUNIA WA BAHARI (2023) ATEMBELEA OFISI ZA MPRU- HQ
MLIBWENDE WA DUNIA WA BAHARI (2023) ATEMBELEA OFISI ZA MPRU- HQ

Tarehe Iliyochapishwa: Alhamisi, Januari 19, 2024

Mlimbwende wa Dunia wa Bahari (Miss Ocean World) 2023 na mshindi wa tatu (3) Mercy Paul ametembelea Ofisi za Makao Makuu ya Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu Tanzania zilizopo Upanga, Dar es Salaam.

Ushiriki wake katika Mashindano hayo, yaliofanyika nchini India na kukutanisha washiriki kutoka Mataifa 43 ni wa kujivunia na wenye tija katika juhudi za kukuza shughuli za Utalii na Uhifadhi wa rasilimali za Bahari duniani kote.

Mercy (22) ni mwanafunzi wa Chuo cha Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) mwaka wa 2 na kwa mara ya kwanza alikuwa Miss Utalii Tanzania 2022, ameipeperusha vyema bendera ya Tanzania katika eneo la Utalii hasa upande wa Bahari.

Kupitia mualiko huo, Mrembo Mercy alipata nafasi ya kuelezea safari yake katika Tasnia ya Mashindano ya Ulimbwende mpaka kufikia mafanikio makubwa ya ushiriki wa ‘Miss World Ocean’ kwa mafanikio makubwa kwa kufanikiwa kuwa mshindi wa (3) duniani. 

 Aidha, Mercy alipata fursa ya kuifahamu MPRU na shughuli zake nzima zinazofanywa za Uhifadhi wa Bahari pamoja na mchango wake yakinifu   katika kukuza uchumi wa Buluu nchini.