WAZIRI KAIRUKI AWATAKA WATALII KUTEMBELEA VISIWA VYA ZANZIBAR, MAFIA, KILWA
WAZIRI KAIRUKI AWATAKA WATALII KUTEMBELEA VISIWA VYA ZANZIBAR, MAFIA, KILWA

Tarehe Iliyochapishwa: Ijumaa, Octoba 06, 2023

Waziri wa Maliasili na Utalii nchini Mhe. Bi. Angellah Kairuki amewataka watalii wa kigeni kufika katika fukwe za Kisiwa cha Zanzibar, Mafia pamoja na Kilwa alipokuwa akihutubia Maonesho ya saba ya Kimataifa ya Utalii nchini (SITE 2023)  katika ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.

Waziri Kairuki ameyasema hayo Leo Octoba 6, 2023 alipokuwa akihutubia  kama mgeni rasmi wa Maonesho haya ya 7 ya Kimataifa ya Utalii nchini.

"Nawashauri watalii msiondoke bila kutembelea baadhi ya vivutio vyetu vya utalii ikiwemo fukwe bora duniani katika Visiwa vya Zanzibar, Mafia pamoja na Kilwa” amesema Mhe. Kairuki.

Aidha, Mhe. Kairuki amewasifia waandaji wa Maonesho haya ya 7 ya Kimataifa ya Utalii kwa ubunifu na mkubwa ambapo kupitia maonesho haya yatasaidia kuitangaza Tanzania kimataifa na kuiweka katika ramani nzuri katika sekta ya utalii kimataifa.

“Ndugu zangu kwa jinsi ambavyo leo nimeshuhudia maonesho haya yalivyofana sitasita kumfahamisha Mhe. Rais wa Jamhuri ya ,Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhusu mambo mazuri yaliyofanyika hapa na kazi kubwa na nzuri ya kutangaza utalii wa nchi yetu inavyoendelea kufanywa na wadau wote wa utalii hapa nchini ikiwa ni pamoja na mchango mkubwa na adhimu unaotelewa na sekta yetu binafsi hapa nchini Tanzania tunawashukuru sana.

Kwa hakika maonesho haya ya SITE 2023 ni kielelezo tosha cha ubunifu lakini vilevile jitihada ambazo tunazifanya ili kuendelea kuiweka Tanzania katika hadhi yake ambayo inastahili hapa ya utalii duniani" aliongezea Mhe. Kairuki. 

Kwa upande wake, Afisa Utalii kutoka Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu nchini Bw. Davis Mpotwa amesema Maonesho haya ya Kimataifa ya Utalii nchini yamesaidia kuongeza wateja wapya wa kigeni vilevile itatoa fursa za uwekezaji kwa upande wa hoteli na usafirishaji katika shughuli za uhifadhi na kuendelea kuhamasisha sera ya uchumi wa bluu nchini.

Katika picha hapo juu ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Mafia Mhe. Olivanus Paul Thomas alipofika kutembelea banda la Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu  leo Octoba 06, 2023.

Katika picha hapo juu ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Mafia Mhe. Olivanus Paul Thomas alipofika kutembelea banda la Hifadhi za Ba

neo Tengefu.l leo Octoba 06, 2023.

 

 

 

Katika picha hapo juu ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Mafia Mhe. Olivanus Paul Thomas alipofika kutembelea banda la Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu.l leo Octoba 06, 2023.