MIMP YAPOKEA MELI KUBWA YA KITALII “THE WORLD CRUISE” ILIYOBEBA WATU 442
MIMP YAPOKEA MELI KUBWA YA KITALII “THE WORLD CRUISE” ILIYOBEBA WATU 442

Alhamisi, 28 Machi 2024, Mafia

Meli kubwa ya kitalii iliyobeba jumla ya watu 442 imetia nanga katika Hifadhi ya Bahari ya Bahari ya Kisiwa cha Mafia (MIMP) iliyopo katika Wilaya ya Mafia ikitokea Moroni, Visiwa vya Comoro.

Meli hiyo ijulikanayo kama "The World " yenye wahudumu wapatao 288 ( crew) na abiria 154 imefika katika eneo la Ras Kisimani Mafia ambapo watalii waliweza kupata burudani kutoka kwa vikundi mbalimbali vya ngoma za asili na kujionea mandhari nzuri.

Akizungumza wakati wa kuwapokea watalii hao, Mkuu wa Wilaya ya Mafia Mhe. Aziza Mangosongo, amedhihirisha kufurahishwa kwake pamoja na kutambua juhudi za Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuitangaza Tanzania.

"Haya ni matokeo ya Royal Tour pamoja na Mafia Island Festival. Sisi kama Mafia tunamshukuru Mhe. Rais kwa kuweza kutufungulia njia na sisi tunaanzaia pale alipoishia yeye" alisema Mhe. Mangosongo.

 Aidha, amesisitiza kuwa Kisiwa cha Mafia ni salama na miundombinu yake imeimarika ikiashiria utayari wake wa kupokea watalii na wawekezaji. 

“Ni mara yangu ya kwanza kufika Mafia na nimeshangazwa na uzuri wake. Kila mtu amefurahi sana hasa mimi ambapo nimeweza kuona tamaduni za watu wa hapa" alisema Alma Martinez, Mhudumu wa meli hiyo, raia wa Mexico.

Kisiwa cha Mafia kina jeografia ambayo ni rahisi kufikika, safu ya vivutio na uoanifu na mapendeleo tofauti ambapo hukifanya kuwa mahali pazuri penye uzoefu wa kukumbwa wa likizo kwa watalii.