MRADI CRR KUWEZESHA UTUNZAJI ENDELEVUWA RASILIMALI ZA BAHARI
MRADI CRR KUWEZESHA UTUNZAJI ENDELEVUWA RASILIMALI ZA BAHARI

Tarehe Iliyochapishwa: Jumatano, Januari 24, 2024

Mkuu Wilaya ya Ilala, Mh. Edward Mpogoro amefungua warsha ya mradi wa Uokoaji wa Miamba ya Matumbawe (Coral Reef Rescue Project) iliofanyika hoteli ya Peacock Januari 23,2024 katika kikao kilichoshirikisha wadau mbalimbali waliolengwa na mradi huo kutoka Tanzania bara na visiwani jijini Dar Es Salaam. Mradi huu utakaotekelezwa na Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU) ambapo unaotarajiwa kuanza hivi karibuni.

Kutokana na  uharibifu wa miamba ya matumbawe kumekuwepo hatari ya kutoweka kwa miamba hio hivyo Mradi wa Coral Reef Rescue ni nyenzo muhimu katika utunzaji na uhifadhi wa matumbawe ambapo ni vivutio, makazi na mazalia ya aina mbali mbali za viumbe wa baharini.

Mradi umelenga kuongeza pato la Taifa kupitia uhifadhi ambapo utawezesha uvuvi endelevu na pia kuongeza fursa za uwekezaji baharini ikiwemo uvunaji wa hewa ukaa pamoja na kukuza utalii wa bahari. Aidha mradi unatarajiwa kuja na suluhu juu ya uvuvi haramu ikiwemo uvuvi kwa kutumia vilipuzi.

Serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali kupitia sekta binafsi na jamii kwa ujumla, wanatarajiwa kushirikiana bega kwa bega katika mradi huu kwa maendeleo endelevu na uhifadhi wa rasilimali za bahari.